IQNA

Hospitali nchini Canada yawapa wagonjwa chakula halali

12:41 - May 06, 2019
Habari ID: 3471944
TEHRAN (IQNA) – Hospitali moja katika eneo la Fort McMurry, mkoani Alberta, nchini Canada imekuwa hospitali ya kwanzake katikaukanda wa Alberta kaskazini kuwapa wagojwa chaguo la chakula halali.

Kituo cha Afya cha Kieneo cha Northern Lights  kilianza kuwapa wagonjwa chakula halali mwezi Novemba mwaka 2018 na hadi sasa wagonjwa 100 wamepata chakula halali.

Bi. Kiran Malik-Khan, mwanachama wa bodi ya afya ya Taasisi ya Afya ya Northern Lights amesema kumekuwepo na pengo hilo la ukosefu wa chakula halali na linapaswa kujazwa.

Ameongeza kuwa eneo la Fort McMurry lina Waislamu takribani 10,000 na hivyo kuwepo udharura wa huduma hiyo.

Bi. Kiran Malik-Khan amesema yamkini Waislau wanaofika katika hospitali hiyo wasijitambulishe kwa sababu mbali mbali au hawana habari kuwa kuna huduma ya chakula halali na kwa msingi hiyo wote wanaofika hospitalini hapo kupata matibabu watajulishwe kuhusu kuwepo chaguo la chakula halali.

Waislamu katika nchi nyingi zisizo za Kiislamu hupata tabu sana kutokana na chakula cha hospitali kutokuwa halali.

Chakula Halal huwa kinatayarishwa kwa kuzingatia mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu.

3468439

captcha