IQNA

Aghalabu ya Waislamu Scotland wamekumbana na chuki dhidi ya Uislamu

23:11 - June 29, 2021
Habari ID: 3474055
TEHRAN (IQNA)- Karibu asilimia 83 ya Waislamu nchini Scotland wameshuhudia vitendo vya moja kwa moja vya chuki dhidi ya Uislamu au Islamophobia.

Jopo la Bunge la Scotland la Kufuatilia Islamophobia limebainisha hayo katika uchunguzi wa tatizo la Islampohobia kote Scotland.

Ripoti iliyochapishwa na jopo hilo inaonyesha asilimia 83 ya Waislamu waliohojiwa na jopo hilo wanasema wameshuhudia chuki dhidi ya Uislamu ambapo wanawake ndio wanaolengwa zaidi.

Aidha Waislamu wengi wanaohujumiwa wanaishi katika mji mkuu wa Scotland, Glasgow. Uchunguzi umebaini kuwa idadi kubwa ya Waislamu wanahujumiwa wanapokuwa wakitumia usafiri wa umma.

Ripoti hiyo imechapishwa na Profesa Peter Hopkins wa Chuo Kikuu cha Newcastle ambaye amekuwa akifanya utafiti kuhusu ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya Uislamu nchini Scotland katika kipindi cha miaka 20.

Amesema ushahidi uliokusanywa unaonyesha kuwa, Scotland ina tatuzi kubwa la ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya Uislamu.

Msemaji wa serikali ya Scotland amesema: “Tunaazma ya kukabiliana na uhalifu ikiwa ni pamoja na chuki dhidi ya Uislamu na tutazingatia mapendekezo ya jopo la uchunguzi.”

3475097/

Kishikizo: scotland waislamu
captcha