IQNA

Sala ya Idul Adha kusaliwa Msikiti wa Al Aqsa

23:29 - July 14, 2021
Habari ID: 3474100
TEHRAN (IQNA)-Sala ya Idul Adha itaswaliwa katika Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) wiki ijayo.

Hayo yamedokezwa na Mufti wa Mji wa Quds Sheikh Muhammad Hussein ambaye amesema wanatazamiwa kusali Sala ya Idi Jumanne Julai 20 kuanzia saa kumi na mbili asubuhi.

Mufti huyo ametoa wito kwa wale wanaotaka kushiriki katika Sala hiyo kuzingatia kanuni za kiafya za kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19.

Aidha ametoa wito kwa wale wenye uwezo kuchinja na kuwasiadia wasiojiweza katika jamii katika siku hiyo ya Idi.

Wapalestina karibu laki moja walishiriki katika Sala ya Idul Fitr mwaka huu katika Msikiti wa al Aqsa ambao ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu katika mji wa Quds (Jerusalem) licha ya sheria kali zilizowekwa na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Katika miaka ya hivi karibuni, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshadidisha hujuma na uvamizi wake dhidi ya maeneo ya Wapalestina ukifanya njama za kufikia malengo yake haramu katika ardhi za Wapalestina.

Msikiti wa al-Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu umekuwa ukiandamwa na njama mtawalia za utawala vamizi wa Israel, hatua ambazo zinakwenda sambamba na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina.

3984105

Kishikizo: sala idi msikiti aqsa
captcha