IQNA

Saudi Arabia yatangaza Umrah imeanza tena, Julai 25.

20:15 - July 25, 2021
Habari ID: 3474126
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa Urais Mkuu wa Maswala ya Misikiti Miwili Mitakatifu amewaamuru wahusika wenye uwezo kukamilisha maandalizi ya kuwapokea waumini wanaotaka kutekeleza Ibada ya Umrah.

Afisa huyo alinukuliwa katika vyombo vya habari vya Saudia akitoa wito kwa wahusika kufanya juhudi zote na kuzingatia hatua zote za tahadhari katika Msikiti Mkuu wa Makka na Msikiti wa Mtume SAW huko Madina.

Naibu Waziri wa Hija wa Saudi na Umrah Abdulfattah Al Mashat hivi karibuni alisema kuwa Umrah itaanza upya mnamo kati kati ya  mwezi wa Kiislamu wa sasa wa Dhu Al Hijjah na vibali vinavyohusiana vinaweza kupatikana kupitia programu mahiri ya Itamarnah.

“Hapo mwanzo, idadi ya wanaotekelelza Ibada ya Umra hitakuwa 20,000 [kwa siku]. Idadi itaongezeka pole pole,” aliiambia runinga inayomilikiwa na Saudi Arabia Al Arabiya.

Mnamo Oktoba, Saudi Arabia ilianzisha mpango wa kuanza tena taratibu kwa Umrah wakati wa tahadhari kali dhidi ya COVID-19.

Kwa sasa kama ilivyokuwa Hija ni Waislamu wanaoishi Saudia tu watakaoruhusiwa kutekeleza Ibada ya umrah.

3475322

Kishikizo: saudi umrah hija
captcha