IQNA

Sherehe za Ghadir zaanza kufanyika Tehran

19:29 - July 26, 2021
Habari ID: 3474128
TEHRAN (IQNA)-Sherehe zimanza kufanyika katika mji mkuu wa Iran, Tehran na mji mtakatifu wa Mashhad kaskazini mashariki mwa nchi kwaa mnasaba wa kukaribia Siku Kuu ya Idul Ghadir.

Kwa kawaida sherehe hizo ambazo hufanyika baina ya Idul Adha na Idul  Ghadir hujulikana kama ‘sherehe za Wilayat’

Waislamu wa madhehebu ya Shia kote duniani wameanza kuaadhimisha sikukuu ya Ghadir ambayo ni kati ya siku muhimu zaidi katika kalenda ya historia ya Uislamu.

18 Dhulhija takribani 1431 iliyopita Mtume Muhammad SAW akiwa katika safari yake ya mwisho ya Hija, kwa amri ya Mwenyezi Mungu alimtangaza Imam Ali bin Abi Twalib AS kuwa kiongozi wa Waislamu wote baada yake.
Hatua hiyo ya Mtume Mtukufu ilifanyika katika eneo linalojulikana kwa jina la Ghadir Khum katika makutano ya njia ya Makka na Madina.  Siku hii huadhimishwa kama  Siku Kuu ya Ghadir.

 
captcha