IQNA

Sayyid Hassan Nasrallah

Ushiriki mkubwa wa Walebanon katika uchaguzi ni uungaji mkono kwa Hizbullah na silaha zake

12:23 - May 20, 2022
Habari ID: 3475268
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, amewashukuru na kuwapongeza watu wote walioshiriki katika uchaguzi wa bunge uliofanyika hivi karibuni na akasema ushiriki mkubwa wa Walebanon katika uchaguzi huo na matokeo yake yamefikisha ujumbe wa uungaji mkono kwa Hizbullah au Muqawama na silaha zake.

Sayyid Hassan Nasrallah ameyasema hayo katika hotuba ya kwanza aliyotoa baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa bunge la Lebanon uliofanyika siku ya Jumapili iliyopita, ambapo kama ilivyotokea katika uchaguzi uliopita, vuguvugu la muqawama liliibuka mshindi.

Amesema vitisho vyote na kila aina ya uenezaji hofu ili kuwafanya wananchi wa Lebanon wasishiriki katika uchaguzi havikuwa na tija yoyote na akaongeza kwamba, mahudhurio makubwa ya Walebanon katika awamu tatu za uchaguzi lilikuwa jibu madhubuti kwa vitisho hivyo.

Kuhusiana na ushindi uliopata Muqawama katika uchaguzi huo wa bunge, Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema: "Sisi tunajivunia ushindi huu mkubwa; na hasa tunapofikiria ni katika mazingira gani ushindi huu umepatikana na kiwango gani cha gharama kimetumika ili kuuzuia."

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Sayyid Hassan Nasrallah amegusia tuhuma kadhaa zisizo na msingi zilizotolewa na baadhi ya watu na mirengo kwamba Iran imeingilia uchaguzi wa Lebanon na akaeleza kwa kuhoji: "Je imewahi kukutokeeni japo mara moja kumshuhudia balozi au mfanyakazi yeyote ya ubalozi wa Iran akiingilia uchaguzi? Hali ya kuwa tumeshuhudia uingiliaji wa ubalozi wa Marekani katika mchakato wa uchaguzi na balozi wa Saudia Arabia ambaye alishughulika mno wakati wa mwenendo wa uchaguzi."

Katika miezi ya karibuni, maadui wa muqawama wamegharimika mno na kufanya kila njia ili kuutoa muqawama kwenye ulingo wa muundo wa kisiasa wa Lebanon.

Talal A'trisi, mchambuzi mashuhuri wa masuala ya kisiasa nchini Lebanon amesema Marekani na waitifaki wake ndio washindwa wakubwa zaidi katika uchaguzi wa Bunge wa Lebanon.

/3478964

captcha