IQNA

Sala ya Ijumaa Tehran

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran: Usalama wa Iran hauwezi kufumbumbiwa macho hata kidogo

20:52 - September 30, 2022
Habari ID: 3475858
TEHRAN (IQNA)- Hatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amepongeza hatua ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ya kushambulia ngome za magaidi wanaotaka kujitenga huko kaskazini mwa Iraq na kusema: Usalama wa Iran hauwezi kufumbumbiwa macho hata kidogo.

Hujjatul-Islam Walmuslimin Mohammad Javad Haj Ali Akbari amesema katika hotuba za Swala ya Ijumaa ya wiki hii mjini Tehran kwamba: “Tunashukuru kwa dhati mashambulizi yaliyofanywa na Sepah dhidi ya magaidi wanaotaka kujitenga kaskazini mwa Iraq, usalama wa nchi hii hauwezi kuchezewa, na makundi haya yanafanya kila aina ya ufisadi dhidi ya usalama wa Iran katika vituo vyao 50 hadi 60 katika eneo la kaskazini mwa Iraq.”

Itakumbukwa kuwa, Vikosi vya Nchi Kavu vya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) vimeanzisha duru mpya ya mashambulio dhidi ya ngome na maficho ya magaidi kwa kutumia makombora ya balestiki huko kaskazini mwa Iraq.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, jeshi la SEPAH limetumia makombora 360 yenye kupiga shabaha kwa usahahi mkubwa katika operesheni hizo dhidi ya ngome na maficho ya magaidi kwa kutumia makombora ya balestiki na droni katika eneo la Kurdistan, kaskazini mwa Iraq.

Amesema ngome 42 za magaidi hao, baadhi zikiwa zimepishana kwa umbali wa kilomita 400 zimesambaratishwa na kuharibiwa kikamilifu na makombora hayo ya balestiki na droni za Iran.

Kuhusu matukio ya hivi karibuni nchini na njama za maadui na wafanya ghasia, Haj Ali Akbari amesema: Kwa kutumia hazina kubwa ya kipindi cha kujitetea kutakatifu, tunaweza kueneza mafundisho ya kujilinda kwa kasi na njia bora zaidi.

Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amepongeza mahudhurio makubwa ya wananchi kwenye maandamano ya Umma wa Muhammad Rasulullah (saw) na kuyataja kuwa yametengeneza hamasa mpya katika kipindi kigumu.

Amesema taifa la Iran linamjua vyema adui na limetanguliza mbele maslahi ya nchi na kujitenga na safu za maadui kwa hamasa kubwa ya tarehe 3 mwezi huu wa Mehr (25 Septemba).

Amesema: Katika mikusanyiko na maandamanao hayo makubwa wananchi walitilia mkazo umoja wao na kutoa wito wa kutolewa adhabu kali kwa wafanya fujo na wale wanaoanzisha fitina nchini kwa niaba ya madola ya kigeni. Amesisitiza kuwa, wananchi wanatarajia kuona mfumo wa mahakama ukiwashughulikia kisheria wahusika wa ghasia na machafuko hayo.

Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran pia amesema wananchi wamelipongeza jeshi la polisi na juhudi zake za kuhakikisha usalama wa nchi, na wanatoa wito kuchunguzwa sababu za kifo cha Mahsa Amini.

Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran pia amekemea vikali hujuma dhidi ya vazi la hijabu la mwanamke wa Kiislamu na kutoa wito kwa Bunge na vyombo vya kutunga sheria kuweka sheria kali za kulinda vazi hilo la mwanamke wa Kiislamu.

4088756

 

4088756

captcha