IQNA

Spika wa Bunge la Iran

Umoja utasuluhisha matatizo ya nchi za Kiislamu

12:52 - December 11, 2021
Habari ID: 3474663
TEHRAN (IQNA)- Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu,Bunge la Iran amesema kuwa umoja ni suluhisho pekee kwa matatizo ambayo yanaukumba umma wa Kiislamu duniani kote.

Muhammad Qalibaf aliyasema hayo jana katika Mkutano wa 16 wa Jumuiya ya Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) uliofanyika nchini Uturuki. Ameongeza kuwa, mshikamano na kushirikiana baina ya Waislamu ni maudhui ya kistratijia ya Umma wa Kiiislamu na kuongeza kuwa, suala hilo muhimu linapaswa kupewa mazingatio maalumu na Jumuiya ya Mabunge ya Nchi za Kiislamu.

Aidha amesema kuwa kadhia ya Palestina ndio kipaumbele kikubwa zaidi cha Ulimwengu wa Kiislamu na kwamba kambi muqawama na mapambano ndiyo sababu na kudhalilishwa na kuchukiwa Wazayuni. Amesisitiza kuwa, kudumishwa njia hiyo kutapelekea kuangazwa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Amesema, katika miongo ya karibuni nchi za Waislamu zilianzisha harakati mpya za ustawi katika nyanja mbalimbali za kiutamaduni, kijamii na kisiasa na kuongeza kuwa, mabadiliko hayo ya taratibu yatazaa matunda ya mustakbali mwema kwa Ulimwengu wa Kiislamu pale mataifa yote ya Waislamu yatakaposhirikiana na kushikamana kwa kutumia maadili ya Kiislamu kwa ajili ya kutatua matatizo ya Umma wa Kiislamu.

Akibainisha kwamba, kadhia ya Palestina ndiyo kipaumbele cha kwanza cha Ulimwengu wa Kiislamu, Muhammad Qalibaf amesema: Imepita zaidi ya miongo saba sasa ambapo dunia inatazama kwa macho tu siasa na ukatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel unaokiuka misingi ya awali kabisa ya haki za binadamu na utu wa Wapalestina. Amesema mapambano yamefelisha mradi na njama za Uzayuni na kwamba muqawama na mapambano si  utamaduni wa kufa, bali ni utamaduni wa kuishi. 

Vilevile ameashiria maudhui ya Afghanistan kama mojawapo ya masuala yanayozusha wasiwasi mkubwa kwa Umma wa Kiislamu na kusema: Kwa miongo kadhaa sasa Iran imethbitisha kuwa, ni mtetezi na mwenyeji bora kwa watu azizi wa Afghanistan na imekuwa ikitoa huduma za kimaisha, afya na elimu kwa zaidi ya wakimbizi milioni 3.5 wa Afghanistan kadiri ya uwezo wake. Hata hivyo amesisitiza kuwa vikwazo vya kidhalimu vilivyowekwa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu vinatatiza suala la kukidhi mahitaji yanayoongezeka kila siku ya wakimbizi hao.   

4019884

 

captcha