IQNA

Balozi wa Saudia nchini India atunukiwa Tafsiri ya Qur'ani ya Kisinhala

19:17 - May 17, 2023
Habari ID: 3477012
TEHRAN (IQNA) – Balozi wa Sri Lanka nchini India Milinda Moragoda amemtunuku Balozi wa Saudia nchini India Saleh Eid Al-Husseini nakala ya tafsiri ya Kisinhala ya Qur'ani Tukufu.

Hatua hiyo ilikuwa ni sehemu ya juhudi zake za kuimarisha mazungumzo na wakuu wa ujumbe wa nchi za Kiislamu mjini New Delhi.

Hafla hiyo ilifanyika Jumanne wakati Moragoda alipokutana na Al- Husseini katika ubalozi wa Saudi Arabia huko New Delhi. Wakati wa mkutano huo, pande hizo mbili zilibadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa ushirikiano wa kiuchumi wa pande tatu kwa ushiriki wa India.

Tafsiri ya Kisinhala ya Qur'ani Tukufu iliyokabidhiwa Balozi wa Saudi imechapishwa na All Ceylon Jamiyyathul Ulama (ACJU) ya Sri Lanka.

Hapo awali, Balozi Moragoda alikuwa amewasilisha Misahafu ya Kisinhala kwa Jama Masjid ya Delhi, Jamiat Ulama-i-Hind (Baraza la Wanatheolojia Waislamu wa India) na pia kwa mabalozi wa Morocco na Bahrain na Balozi wa Nigeria mjini New Delhi.

Amekuwa akikuza mazungumzo na dini zote kuu nchini India, kwa kuzingatia  sera ya "Mkakati wa Ushirikiano wa Ofisi za Kidiplomasia za Sri Lanka nchini India".

3483593

Kishikizo: sri lanka india waislamu
captcha