Aidha waandamanaji hao wametaka misaada ya kibinadamu ifikiswhe Gaza haraka ili kuokoa maisha ya watu akribu milioni mbili wa eneo hilo.
Hafla hiyo, iliyoandaliwa na Muungano wa Palestina, ilikuwa ni sehemu ya kampeni ya kimataifa ya kuonyesha mshikamano na watu wa Palestina na kuishinikiza serikali ya Marekani kuchukua hatua kukomesha vita.
"Yote ni juu ya kukusanyika kama jamii kutoa wito wa kusitishwa kwa mapigano, kuachiliwa kwa mateka na wafungwa wote, kufikishwa msaada wa kibinadamu Gaza na kuweka shinikizo kwa viongozi wetu waliochaguliwa, wafanye kuunga mkono azimio la kusitisha mapigano na kuonyesha mshikamano na watu wa Palestina,” alisema Brendan Davison, mratibu wa muungano huo.
Renae Al-Fdeilat, mwanajamii aliyehudhuria hafla hiyo, alisema yeye ni mke wa Mpalestina na mama wa watoto wa Kipalestina, na kwamba ana familia katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu. Alisema hujitahidi kuwasiliana nao kila siku kuwajulia hali.
Utawala wa Kizayuni wa Israel kwa himaya ya Marekani ulianzisha vita vya kikatili huko Gaza mnamo Oktoba 7 kufuatia operesheni ya kihistoria ya kundi la wanamapambano ya Kiislamu la Palestina, Hamas, dhidi ya utawala wa Kizayuni ambao umekuwa ukiwakandamiza wa Palestina kwa zaidi ya miongo saba.
Hadi sasa utawala katili wa Israel umeua Wapalestina wasiopungua 26,422, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na kuwajeruhi wengine wasiopungua 65,087.
3486999