Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, aliyasema hayo jana Alkhamisi katika mkutano na Ziyad al-Nakhala, Katibu Mkuu wa Harakati ya kupigania ukombozi wa Palestina au muqawama ya Jihad Islami pamoja na ujumbe aliofuatana nao.
Aliashiria jinai za utawala wa Kizayuni wa kuwaua watu wa Gaza na akasema, ukiona utawala wa Kizayuni ulio na kila aina ya zana za kijeshi huku ukiungwa mkono na madola ya kidhalimu duniani unaua wanawake na watoto, hiyo ni ishara kwamba utawala huo hauna uwezo wa kukabiliana na vikosi vya Muqawama na kuvishinda.
Ayatullah Khamenei amemhutubu Katibu Mkuu wa Jihadul-Islami na kusema: "kwa rehema za Mwenyezi Mungu mutauona ushindi kamili wa watu wa Gaza".
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Jihadul-Islami ya Palestina ameshukuru na kuthamini uungaji mkono wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kadhia ya Palestina, na akaienzi kumbukumbu ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani kamanda wa zamani wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) aliyeuawa shahidi na akasema: "licha ya shida na njama zote, watu wa Ghaza wakiwa bega kwa bega na vikosi vya Muqawama, wameweza -kwa kusimama kwao imara kusio na kifani- kuushinda mpango wa Marekani na utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wao wa kutaka kuuangamiza Muqawama".
Ziyad al-Nakhala amesema kuna uratibu kamili kati ya vikosi vya Muqawama hususan baina ya Hamas na Jihadul-Islami na akaongeza kuwa: watu wa Gaza na vikosi vya Muqawama wameazimia kwa dhati kuendeleza istikama na kusimama imara hadi ushindi kamili; na kwa rehma za Mwenyezi Mungu, ushindi kamili utapatikana katika muda si mrefu ujao.
Siku ya Jumanne, Machi 26, Ismail Haniya, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina HAMAS na ujumbe aliofuatana nao walikutana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Katika mkutano huo Ayatullah Khamenei alipongeza istikama na kusimama imara kusio na mfano kulikooneshwa na vikosi vya Muqawama na vilevile watu wa Gaza na akasisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitasita hata chembe kuunga mkono kadhia ya Palestina na wananchi wanaodhulumiwa na wastahamilivu wa Gaza.
Mikutano hiyo imefanyika katika hali ambayo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hivi karibuni limepitisha azimio la kusitishwa vita haraka huko Gaza.
3487740