IQNA

Kiongozi Muadhamu Azuru Haram ya Imam Khomeini (quddisa sirruh)

9:54 - January 29, 2015
Habari ID: 2777820
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Jumatano amekwenda kufanya ziara katika Haram ya mwanachuoni huyo mkubwa, na sambamba na kumsomea Faatiha, amemuenzi na kumuombea dua mwasisi huyo wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Ziara hiyo imekuja zikiwa zimekaribia siku za Mwenyezi Mungu za Alfajiri Kumi za maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran yanayoanzia siku aliporejea kishujaa nchini Iran, Imam Khomeini-Mwenyezi Mungu Amrehemu.

Vile vile Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amefanya ziara kwenye maziara ya mashahidi wa Tir 7 (kwa mwaka wa Kiirani wa Hijria Shamsia) na kwenye makaburi ya mashahidi wengine ya Behesht Zahra (kusini mwa Tehran), na kuwaombea dua kwa Mwenyezi Mungu awapandishe daraja za juu mbele Yake.
Itakumbukwa kuwa siku ya Alkhamisi ya Februari 1, 1979, Imam Khomeini (quddisa sirruh) alirejea nchini Iran kutoka ubaidishoni nchini Ufaransa, na kurejea kwake huko kulitia nguvu harakati za mapinduzi ya wananchi wa Iran yaliyoung'oa madaraka utawala wa kidikteta wa Shah, Februari 11, 1979.
Siku hizo kumi za baina ya kurejea nchini Iran Imam Khomeini (quddisa sirruh) hadi kupatikana ushindi kamili wa Mapinduzi ya Kiislamu ni maarufu kwa jina la Dahe Fajr yaani Alfajiri Kumi na huadhimishwa kila mwaka. Sherehe hizo hufikia kileleni Februari 11, siku ambayo ni maarufu kwa jina la Bahman 22.../mh

2773548

captcha