IQNA

Wananchi wa Iran waadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu

21:45 - February 11, 2015
Habari ID: 2840030
Mamillioni ya wananchi wa Iran leo wamejitokeza na kushiriki kwa wingi katika maandamano ya kuadhimisha mwaka wa 36 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Katika maandamano hayo ya mamilioni ya wananchi wa Iran, waandamanaji wa kada mbalimbali wameshiriki kwa wingi na kwa hamasa kubwa wakiwa wamebeba bendera za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huku wakipiga nara kama "nishati ya nyuklia ni haki yetu ya wazi",  "damu katika mishipa yetu ni zawadi kwa kiongozi wetu", mauti kwa Marekani” na , "mauti kwa Israel".
Sherehe za kuadhimisha mwaka wa 36 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini Iran zimehudhuriwa pia na wageni zaidi ya 400 kutoka nchi zaidi ya 30 duniani. Maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu mwaka huu pia yamehudhuriwa na waandishi habari wa nchi za nje zaidi ya 265. Maandamano hayo yameakisiwa na vyombo vya habari kote duniani huku baadhi ya kanali za televisheni na radio zikitangaza moja kwa moja hotuba ya Rais Hassan Rouhani katika maandamano hayo.
Baada ya kumalizika maandamano hayo wananchi walioshiriki kwa pamoja wametoa taarifa na kusisitiza kuwa hakuna mazungumzo yoyote yatakayofanyika kuhusu mafanikio ya Iran katika sekta ya ulinzi hasa kuhusu makombora ya kujihami. Aidha wametilia mkazo ulazima wa kutekelezwa wasia wa Imam Khomeini Mwenyezi Mungu amrehemu na nasaha za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu huku wakisisitiza kuhusu umoja wa taifa lote la Iran.../mh

2836924

captcha