Kwa mujibu wa taarifa, kutakuwa na jumla ya washiriki 631 watakaoshindana katika kageoria mbali mbali za mashindano hayo ya Qur'ani ya kimataifa.
Mashindano ya mwaka huu yatakuwa na kitengo cha kawaida cha wanaume na kisha kutakuwa na vitengo maalumu vya wanawake, watu wenye ulemavu wa macho, wanafunzi wa vyuo vya kidini na wanafunzi wa shule.
Halikadhalika amesema kitengo cha wenye ulemavu wa macho kitakuwa na mashindano ya kuhifadhi Qur'ani pekee huku vitengo vikingine vilivyosalia vikiwa na mashindano ya kuhifadhi Qur'ani na kusoma kwa tajwidi.
Fainali za Mashindano ya 36 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu zimepangwa kuanza mjini Tehran kuanzia Aprili 10 katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini mjini Tehran.
Shirika la Wakfu la Iran huandaa mashindano ya kimatiafa ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani ya Iran kila mwaka ambapo huwa na washiriki kutoka kila kona ya dunia.
Mwaka jana kulikuwa na washiriki 370 wa kigeni waliohudhuria mashindano ya kimataifa ya Qur'ani.