IQNA

Wasyria wapiga kura katika uchaguzi wa rais

22:08 - May 26, 2021
Habari ID: 3473948
TEHRAN (IQNA)- Rais Bashar al Assad wa Syria amejiunga na mamillioni ya Wasyria katika kupiga kura katika uchaguzi wa rais nchini humo.

Baada ya kupiga kura, Rais Bashar al Assad ambaye anatetea nafasi yake, amesema watu wa Syria wameungana katika vita dhidi ya ugaidi. Aidha amesema watu wa Syria wamepuuza madai ya nchi za Magharibi kuhusu uchaguzi kwani matamshi wanayotoa hayana maana hata kidogo.

Rais Assad amepiga kura katika mji wa Douma na kusema kuwa hatua yake ya kuutembelea mji huo na kupiga kura mjini humo ni ishara ya wazi ya umoja wa maeneo na makabila yote ya Syria.

Bashar al-Assad anatazamiwa kushinda muhula huu wa nne wa miaka saba ya urais katika uchaguzi ambao unamshirikisha naibu waziri wa zamani Abdullah Sallum Abdullah na Mahmoud Ahmad Marei, ambaye ni mkuu wa Shirika la Kiarabu la Haki za Binadamu.

Mwaka 2014, al Assad alipata asilimia 89 ya kura zote zilizopigwa katika uchaguzi ambao asilimia 73 ya waliotimiza masharti ya kupiga kura walishiriki.

Syria imealika waangalizi wa kimataifa wa uchaguzi kutoka nchi rafiki kama vile Iran na Iraq kwa lengo la kushuhudia upigaji kura unavyofanyika.

Jana mawaziri wa mambo ya nje ya Ufaransa, Ujerumani, Italia, Uingereza na Marekani walidai kuwa uchaguzi huo hautakuwa huru wala haki.

Hii ni katika hali ambayo nchi hizo za Magharibi zikishirikiana na tawala vibaraka katika eneo zilituma magaidi wakufurishaji Syria mwaka 2011 ambao walianzisha vita kwa lengo la kuiangusha serikali halali ya Rais Assad.

Hata hivyo njama hiyo imesambaratika kutokana na oparesheni za jeshi la Syria kwa kushirikiana na harakati za muqawama na washauri wa kijeshi kutoka Iran na Russia.

3474818

captcha