IQNA

Haniya aitaka Saudia iwaachilie huru wafungwa Wapalestina

21:59 - August 05, 2021
Habari ID: 3474161
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ameitaka Saudi Arabia iwaachilie huru mahabusu wote Wapalestina inaowashikilia na kufunga faili lao.

Ismail Haniya ametoa wito huona kueleza kwamba, ana matumaini kwamba, watawala wa Saudia watatangaza tarehe maalumu ya kusikilizwa kesi ya mahabusu wa Kipalestina na mahakama husika ifanye kikao na kutoa hukumu ya kuwaachilia huru mahabusu wote wa Kipalestina.

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Hamas  amesema kuwa: Tunasubiria hukumu ya mahakama na tangazo la kuachiliwa huru wafungwa wa Kipalestina walioshikiliwa katika magereza ya Saudi Arabia.

Hukumu ya wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa huko Saudia inatarajiwa kutolewa Jumapili na Alkhamisi za wiki ijayo.

Watawala wa Saudi Arabia na licha ya matakwa ya kila mara ya Hamas, asasi za haki za binaadamu na familia za watu wanaoshikiliwa huko Saudia, bado wamekataa kuwaachilia huru Wapalestina hao.

Tangu mwaka juzi, Saudi Arabia imewatia mbaroni zaidi ya Wapalestina na Wajordan 60 kwa tuhuma zinazohusiana na kuwa wanachama wa Hamas.

3988593

Kishikizo: hamas palestina saudia
captcha