Maandishi ya nukta nundu hutumiwa na watu wenye ulemavu wa macho.
Mwanachama mwandamizi wa jumuiya hiyo, Mubarak al Hayan amesema Juzuu ya 30 ya Qur’ani Tukufu ambayo pia ni maarufu kama Juzu Amma, imechapishwa kwa maandishi ya nukta nundu kwa kushirikiana na Kituo cha Walemavu wa Macho Kuwait.
Amesema nakala hizo maalumu za Juzu Amma zitasambazwa kwa wale wenye ulemavu wa macho nchini humo na maeneo mengine duniani.
AL Hayan amesema wanapanga kuchapisha vitabu vingine vya Kiislamu na Sunnah ya Mtume Muhammad SAW kwa kutumia maandishi ya nukta nundu.