IQNA

Ghannouchi asema atajiuzulu iwapo hilo litatatua matatizo ya Tunisia

18:08 - November 10, 2021
Habari ID: 3474536
TEHRAN (IQNA) – Spika wa bunge lililosimamishwa kazi la Tunisia amesema atajiuzulu iwapo hilo litatatua matatizo ya kisiasa nchini Tunisia.

Katika mahojiano na gazeti la Al Sabah, Rached Ghannouchi amesema, "Iwapo kujiuzulu kwani ni suluhisho, basi sitasita kufanya hivyo."

Ameongeza kuwa, "Tunakabiliwa na machaguo mawili, ima rais afute maamuzi yake au mgogoro uliopoe utaendelea. Amesema suluhisho la mgogoro wa sasa ni rais kufungamana na katiba kikamilifu.

Ikumbukwe kuwa Julai 25, Rais Kais Saied wa Tunisia alitumia kipengele cha 80 cha katiba ya nchi hiyo kumfuta kazi waziri mkuu Hicham Mechichi, na kulivunja bunge na kujiteua kama kiongozi wa serikali.

Alichukua maamuzi hayo baada ya maandamano kuibuka katika miji kadhaa ya Tunisia kukosoa hali mbaya ya kiuchumi. Waandamanaji hao ambao walikuwa wakimuunga mkono Rais Saied walitaka bunge livunjwe.

Vyama vingi vya kisiasa Tunisia vililaania hatua ya Rais Saied na kuitaja kuwa ni mapinduzi dhidi ya katiba na mafanikio ya mapinduzi yam waka 2011.

3476431

captcha