IQNA

Lita milioni 1.2 za maji ya Zamzam zimesambazwa Makka

20:16 - November 13, 2021
Habari ID: 3474552
TEHRAN (IQNA)- Zaidi ya lita milioni 1.2 za maji ya Zamzam zimesambazwa miongoni mwa wanaofanya ziara katika Msikiti Mtakatifu wa Makka (Masjid al-Haram) katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

Idara ya Usimamizi wa Misikiti Miwili Mitakatifu ya Makka na Madina iimesema lita y1,205,600 za maji ya Zamzam zimesambazwa kwa wale anaotekeleza ibada ya Hija Ndogo ya Umrah na wengine wanaofika katika Msikiti Mtakatifu wa Makka kutekeleza Ibada katika robo ya kwanza ya mwaka huu wa 1443 Hijria Qamaria kuanzia Muharram hadi Rabiul Awwal.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Kusimamia Maji ya Zamzam, Ahmad Bin Shanbar al Nadawi amesema katika kipindi hicho, chupa milioni sita za maji ya Zamzam zimesambazwa Masjid al-Haram.

Machi 2020, Saudia ilisitisha ugawaji maji ya Zamzam kama hatua ya kuzuia kuenea COVID-19. Hatahivyo sasa zoezi za kusambaza maji hayo matakatifu limeanza tena.

Maji yanayotoka katika visima vya Zamzam vinavyopatikana katika Msikiti Mtakatifu wa Makka yana utukufu na baraka telele na hivyo kila anayetembelea msikiti huo mtakatifu hujitahidi kuyapata maji hayo kwa ajili ya kunywa na kuwapelekea wengine kama zawadi.

3476445

 

captcha