IQNA

Mashindnao ya Qur'ani

Mashindano ya kuhifadhi Qur’ani ya kitaifa yafanyika Ethiopia

20:50 - February 26, 2023
Habari ID: 3476630
TEHRAN (IQNA) – Toleo la 4 la Mashindano ya Kitaifa ya Qur’ani Tukufu nchini Ethiopia yaliandaliwa katika mji mkuu wa Addis Ababa siku ya Jumamosi.

Wagombea 50 kutoka sehemu mbalimbali za nchi hiyo ya mashariki mwa Afrika walishiriki katika hafla hiyo ya Qur'ani.

Ilijumuisha kategoria kadhaa za kuhifadhi Qur’ani Tukufu kwa  kuzingatia sheria za Tajweed na Tartil.

Tawi la Ethiopia la Wakfu wa Mohammed VI wa Ulamaa wa Kiafrika limeandaa shindano hilo.

Washindi watashiriki katika hafla mashindano ya  Qur'ani  bara zima la Afrika ambayo yatahudhuriwa na wawakilishi kutoka nchi kadhaa za Kiafrika.

Mashindano hayo yanalenga kukuza shughuli za Qur'ani na kuwahimiza vijana kujifunza na kutekeleza mafundisho ya Kiislamu.

Pia ni fursa ya kutambua vipaji na uwezo wa vijana katika nyanja za Qur'ani, kwa mujibu wa Mohammed al-Rafaqi, katibu mkuu wa Wakfu wa Mohammed VI wa Ulamaa wa Kiafrika

Wakfu wa Mohammed VI wa Ulamaa wa Kiafrika, kwa mujibu wa waanzilishi wake, ni taasisi ya kidini ya Kiislamu inayotaka kuzuia itikadi kali na kukabiliana na malumbano ya kimadhehebu baina ya Waislamu.

Lengo la msingi ni kuunganisha na kuratibu juhudi za wasomi wa Kiislamu kutoka Morocco na nchi nyingine za Afrika ili kuhimiza umoja na uvumilivu pamoja na utafiti wa kina wa mafunzo ya Kiislamu.

3482615

captcha