iqna

IQNA

icc
Jinai za Isarel
TEHRAN (IQNA) - Takriban Wapalestina 74 waliokuwa wakishikiliwa katika jela za utawala wa Kizayuni wa Israel wamekufa shahidi kutokana na kunyimwa huduma kiafya.
Habari ID: 3476287    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/12/22

Jinai za kivita za Israel
TEHRAN (IQNA)- Mashirika kadhaa ya kutetea haki za Wapalestina yameikabidhi Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) maelezo ya kina kuhusu jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu zilizofanywa na utawala wa Israel wakati wa hujuma zake za kijeshi dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza mwaka 2021.
Habari ID: 3475294    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/25

TEHRAN (IQNA)- Jopo la kisheria lililojumuisha mawakili walioko London ambao wanawakilisha waathirika wa mgogoro wa miaka mingi wa Yemen wametaka uchunguzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kuhusu uhalifu wa kivita uliotekelezwa na muungano unaoongozwa na Saudi Arabia katika nchi hiyo masikini zaidi katika Bara Arabu.
Habari ID: 3474244    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/08/31

TEHRAN (IQNA)- Utawala haramu wa Israel umempkonya Riyadh al-Maliki, Waziri wa Mambo ya Nje wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina kibali maalumu kinachotumiwa na viongozi mashuhuru wa Palestina kuvuka mpakani, alipokuwa akirejea katika Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan baada ya kufanya kikao na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC iliyo na makao makuu yake mjini The Hague Uholanzi.
Habari ID: 3473753    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/03/22

TEHRAN (IQNA)- Mwendesha Mashtaka wa Makakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) amesema kuwa mahakama hiyo imeanza uchunguzi kuhusu jinai za kivita zilizofanywa na Israel dhidi ya Wapalestina.
Habari ID: 3473702    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/03/04

TEHRAN (IQNA) – Uamuzi wa hivi karibuni wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) wa kuchunguza jinai za Israel dhidi ya Wapalestina umeungwa mkono na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) na chuo cha Kiislamu cha Al-Azhar nchini Misri.
Habari ID: 3473631    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/08

TEHRAN (IQNA)- Kumekuwa na hisia mseto baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC kutoa hukumu kwa manufaa ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.
Habari ID: 3473626    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/06

TEHRAN (IQNA) -Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina imeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) ichukue hatua za haraka za kuchunguza jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel hasa kitendo cha utawala huo kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.
Habari ID: 3473024    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/02

TEHRAN (IQNA) –Tume ya Kiislamu ya Haki za Binadamu (IHRC) yenye makao yake London, Uingereza imeitaka serikali ya nchi hiyo imuachilie huru mara moja mwanazuoni wa Kiislamu nchini humo, Sheikh Ibrahim Zakzaky na mke wake ambao wamekuwa wakishikiliwa kizuizini tokea mwaka 2015 kwa mashtaka yasiyo na msingi.
Habari ID: 3473012    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/07/29

TEHRAN (IQNA) -Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (HAMAS imeunga mkono uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai unaonyesha kuwa hulka ya uvamizi na ukaliaji ardhi kwa mabavu ya Israel na kiwango cha dhulma ilizowafanyia wananchi madhulumu wa Palestina vimezidi kudhihirika mbele ya jamii ya kimataifa.
Habari ID: 3472297    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/23

TEHRAN (IQNA) – Mwendesha Mashtaka Mkuu katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) amesema ataanzisha uchunguzi kamili kuhusu jinai za kivita za utawala dhalimu wa Israel dhidi ya Wapalestina.
Habari ID: 3472293    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/21

Ujumbe maalumu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) unaelekea ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) ili kuchunguza jinai za kivita zilizofanywa na utawala haramu wa Israel katika vita vya siku 50 dhidi ya Ukanda wa Ghaza.
Habari ID: 3470548    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/09/04

Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Kiislamu ya Uingereza imetangaza kuwa faili la mauaji ya Waislamu katika mji wa Zaria nchini Nigeria limewasilishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu huko The Hague nchini Uholanzi.
Habari ID: 3470211    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/03/23

Jumuiya ya Waislamu wa Kishia Tanzania, AfroShia Muslim Community, inapanga maandamano ya amani kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Quds kwa lengo la kulaani jinai dhidi ya Wapalestina na pia kuunga mkono jitihada za amani duniani.
Habari ID: 3322431    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/07/03