IQNA

Mahujaji wapata mafunzo ya kukabiliana na Ebola

19:25 - September 16, 2014
Habari ID: 1450843
Wizara ya Afya ya Saudi Arabia imeanzisha kampeni maalumu ya kukabiliana na ugonjwa hatari wa Ebola katika kipindi hiki cha kuanza msimu wa Hija.

Wizara hiyo inasambaza vijitabu maalumu kwa mahujaji kuhusu ugonjwa wa Ebola ili kuzuia kuenea ugonjwa huo katika wakati huu ambao mahujaji wameanza kuingia Saudi Arabia. Msemaji wa Wizara ya Afya ya Saudia Khalid Al-Mirghalani amenukuliwa akisema kuwa wizara yake pia imetuma vijitabu hivyo kote duniani ili mahujaji wa mwaka huu waweze kuvisoma kabla ya kuelekea Saudia. Vijitabu hivyo vinatoa maelezo ambayo yanapaswa kufuatwa na mahujaji wakati wakiwa katika miji mitakatifu ya Makkah na Madinah. Saudi Arabia tayari imetangaza kuwazuia mahujaji kutoka nchi zilizoathiriwa zaidi na Ebola ambazo ni Sierra Leone, Liberia na Guinea. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), zaidi ya watu 2,300 wamekwishapoteza maisha kutokana na ugonjwa huo, huko magharibi mwa Afrika.

1450628

Kishikizo: hija saudia makkah madinah
captcha