IQNA

Turathi

Mradi wa ensaiklopidia unalenga kuandika historia ya Hija

20:10 - February 02, 2024
Habari ID: 3478292
IQNA - Mradi wa ensaiklopidia unatekelezwa ili kuweka kumbukumbu za historia ya Hija na Misikiti Miwili Mitukufu (Msikiti Mkuu wa Makka na Msikiti wa Mtume huko Madina) kutoka enzi ya kabla ya Uislamu hadi leo.

Mwanamfalme wa Saudia Faisal bin Salman, mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Wakfu wa Mfalme Abdulaziz wa Utafiti na Hifadhi ya Nyaraka (Darah), alikagua mradi wa Ensaiklopidia  ya Hija ya Misikiti Miwili siku ya Jumatano.

Alikuwa amefuatana na Sheikh Abdullah bin Sulaiman Al-Manea, mjumbe wa Baraza la Wanachuoni Wakuu na mshauri wa Kasri  ya Kifalme.

Mradi huu, unaosimamiwa na Darah, unatumika kama ensaiklopidia kuhusu Hija na Misikiti Miwili Mitakatifu katika vipindi tofauti vya kihistoria.

Wakati wa ukaguzi huo, Faisal na Al-Manea walipokea maelezo ya kina ya malengo ya mradi huo. Mpango huo unalenga kufuatilia kwa makini na kuandika historia ya Hija katika Misikiti Miwili Mitakatifu kutoka enzi ya kabla ya Uislamu hadi siku ya leo.

Zaidi ya hayo, mradi unaangazia maendeleo yaliyofanywa katika kutoa huduma kwa Mahujaji.

3487049

Kishikizo: hija saudia historia
captcha