IQNA

Kiongozi wa Ansarullah

Makka si milki ya Saudia iwazuie mahujaji Wayemen

14:33 - September 21, 2015
Habari ID: 3365868
Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah nchini Yemen ameashiria hatua ya Saudi Arabia ya kuwazuia mahujaji kutoka Yemen kushiriki katika ibada ya Hija na kusema, ‘Makka si milki ya Aal Saudi iwazuie mahujaji wa Yemen.’

Katika hotuba kwa njia ya televisheni Jumapili usiku, Sayyid Abdul Malik Houthi amesema Saudia imekiuka thamani zote za maadili na ubinadamu katika hujuma yake Yemen na imeendeleza maovu yake kwa kuwazuia mahujaji kutoka Yemen kushiriki katika ibada ya Hija mwaka huu. Amesema utawala wa Saudi Arabia umeingiza hitilafu za kisiasa katika ibada ya Hija na kwamba hatua hii itakuwa na athari mbaya katika siku za usoni. Katika hotuba hiyo aliyoitoa kwa mnasaba wa kuwadia mwaka moja tangu kuanza mapinduzi ya wananchi wa Yemen Septemba 21 mwaka 2014, Abdul Malik Houthi amesema taifa la Yemen litaendeleza harakati za kimapinduzi hadi kupatikane ushindi. Ameongeza kuwa ufisadi na udikteta Yemen ndio chanzo cha kuanza harakati ya kimapinduzi ya wananchi na kuongeza kuwa utawala uliopita wa Yemen ulikuwa umegeuka na kuwa kikaragosi cha madola ya kigeni. Kiongozi wa Ansarullah amesema madola ya kigeni yanataka kupora utajiri wa Yemen lakini kwamba Wayemen wako macho na hawataruhusu hilo. Abdulmalik Houthi amesema ufalme wa Saudi Arabia unaangamiza umma wa Kiislamu kwa kueneza fitina mbali mbali ili Waislamu washindwe kukabiliana na utawala wa Kizayuni.../mh

3365603

captcha