IQNA

Maafisa wa utawala Saudia wanatumia Hija kufanya biashara ya mihadarati

20:05 - July 06, 2016
Habari ID: 3470436
Maafisa wa ngazi za juu katika ufalme wa Saudi Arabia wamekuwa wakiingiza dawa za kulevya nchini humo kwa kutumia mabasi yanayowabeba mahujaji, imefichuliwa.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, afisa wa kijeshi mwenye cheo cha meja ambaye aliwahi kufanya kazi katika Idara ya Kupambana na Mihadarati ya Wizara ya Mambo ya Ndani amekamatwa baada ya kufichua kuhusu mtandao huo wenye nguvu wa uingizaji dawa za kulevya Saudia.

Meja Turki bin Hamza al-Rashidi amesema kuwa, mtandao wenye nguvu wa watu walio karibu na watawala wa kifalme Saudia wametengeneza mabilioni ya dola kwa kuingiza dawa za kulevya Saudia kwa njia mbali mbali.

Katika jumbe kadhaa alizotuma katika mtandao wa Youtube, Meja Rashidi anasema kuwa moja ya mbinu iliyokuwa ikitumiwa ni ile ya "mchezo wa mabasi pacha." Mbinu hiyo ilikuwa inahusisha basi lililojaa Mahujaji wa kawaida waliokuwa wakielekea Makka kwa ajili ya Ibada ya Hija. Mabasi hayo yalikuwa yakipita eneo la forodha mpakani na kupewa nyaraka za kuidhinisha kuwa wasafiri na mizigo ni ya mahujaji. Nyaraka hizo hizo zilikuwa zikitumiwa baadaye kuruhusu basi lilolojaa mihadarati kuingia katika ufalme huo.

Meja al-Rashidi anasema mbinu hiyo imekuwa ikitumika kwa miongo kadhaa na kwamba mamia ya mabasi yametumiwa katika maelfu ya safari za kuingiza dawa za kulevya Saudia. Ameongeza kuwa fedha za usafirishaji mihadarati huingia katika mfumo wa kifedha kama fedha zitokanazao na huduma za Ibada ya Hija.

Meja Rashidi anasema katika kazi yake, alifanikiwa ushahidi uliowahusisha maafisa wa ngazi za juu katika Ufalme wa Saudia katika kashfa hiyo ya kutumia mabasi ya Mahujaji kuingiza mihadarati katika ufalme huo. Anasema wakati alipowasilisha ripoti kwa maafisa walio juu yake, kulianzishwa kampeni ya kumtisha na kisha akahamishwa kuenda kuhudumu katika kituo cha mbali sana katika mpaka wa kaskazini mwa Saudia. Amebaini kuwa, baada ya hapo alifutwa kazi kwa madai bandia na tayari ameshatiwa mbaroni huku akihofia maisha yake. Mwezi Oktoba mwaka jana, Mwanamfalme Abdel Mohsen bin Walid bin Abdulazizi kutoka ukoo wa kifalme wa Aal Saud alitiwa mbaroni katika Uwanja wa Ndege wa Beirut Lebanon akiwa na shehena kubwa ya mihadarati aina ya captagon na cocaine katika ndege yake binafsi.

3513368

captcha