IQNA

Mahujaji 410,000 zaidi katika Ibada ya Hija mwaka huu

21:49 - August 29, 2017
Habari ID: 3471148
TEHRAN (IQNA)-Idadi ya Mahujaji mwaka ni 410,000 zaidi ya waka uliopita huku Waislamu kutoka kila kona ya dunia wakiwa katika mji mtukufu wa Makka kutekeleza ibada hiyo ya kila mwaka.
Mahujaji 410,000 zaidi katika Ibada ya Hija mwaka huuKwa mujibu wa Jenerali Sulaiman Abdul Aziz al-Yahya, mkuu Idara ya Pasi za Kusafiria Saudia, mahujaji Milioni 1.73 kutoka nchi mbali mbali duniani wamewasilia Saudia kwa ajili ya Ibada ya Hija.

Amesema Aghalabu ya mahujaji wa kigeni, yaani zaidi ya 1,631,000 wamewasilia nchini humo kwa ndege huku waliosalia wakiwasilia kwa nchi kavu au bahari.

Kwa mujibu wa Idara ya Hija Saudi Arabia, Indonesia ndio nchi yenye idadi kubwa zaidi ya Mahujaji mwaka huu wa 1438 Hijria sawa na 2017 Miladia. Inatazamiwa kuwa Waindonesia 221,000 watatekeleza ibada ya Hija mwaka huu. Indoneisa iko Kuisni Mashariki mwa Asia na ina idadi ya watu milioni 261 na hivyo kuifanya kuwa nchi ya Kiislamu yenye idadi kubwa zaidi ya watu duniani. Nchi zingine zenye idadi kubwa ya Mahujaji ni Pakistan (179,210), India (170,000), Bangladesh (128,000), Nigeria (95,000) na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (86,500).

Mahujaji kutoka nchi za kigeni na wanaoishi ndani ya Saudia mwaka huu wanakadiriwa kuwa milioni mbili.

3635775

captcha