Foroughi ni baba mkarimu ambaye hutumia wakati wake mwingi kusoma Qur’ani na hivyo amewezea kupata sifa ya ukarimu.
Mke wake na watoto wake nao pia humfuata katika kuhakikisha maisha yao yanaenda sambambamba na mafundisho ya Qur’ani Tukufu kama ambavyo pia wagonjwa anaowahudumia hunufaika pia na ucha Mungu wake.
Muuguzi huyo maarufu wa Iran ameweka historia katika Michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020 baada ya kupta medali ya dhahahbu jana katika mashindano ya kulenga shabaha kwa bunduki umbali wa mita 10 shindano la wanaume. Punde baada ya kushinda medali hiyo, Froughi alisujudu na kumshukuru Allah SWT kwa taufiki aliyopata.
Hii ni medali ya kwanza ya Iran katika shindano ya kulenga shabaha kwa bunduki katika Olimpiki.