IQNA

Waislamu Uingereza

Scotland kukabiliana na tatizo linaloongezeka la chuki dhidi Uislamu

18:46 - December 15, 2022
Habari ID: 3476253
TEHRAN (IQNA)-Katika mkutano kamili wa Baraza la Serikali za Mitaa la Eneo la Scotland, la Uingereza wiki iliyopita, diwani Ali Salamati (Kilbride Magharibi Mashariki) alileta hoja ya kuitaka mamlaka ya eneo hilo azimio la kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu au Islamophobia.

Hoja hiyo mbali na kutaka ufafanuzi kamili wa maana ya 'Islamophobia' ilitaka baraza hilo kurejesha dhamira yake ya kupinga ubaguzi wa rangi na ubaguzi wa aina zote na kuunga mkono na kuendeleza Mwezi wa Uhamasishaji kuhusu Uislamu mwezi Novemba kila mwaka.

Hoja hiyo imetaka itambuliwa rasmi kuwa, : "Chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) ina mizizi katika ubaguzi wa rangi na ni aina ya ubaguzi wa rangi unaolenga wale wanaojitangaza kuwa ni Waislamu au wanaoonekana kuwa ni Waislamu".

Diwani Ali Salamati, aliwasilisha mapendekezo hayo, na akasema: “Nimefurahi kuwasilisha hoja ya chama cha SNP na kupitishwa kwa ufafanuzi kuhusu Chuki dhidi Uislamu.

"Idadi ya Waislamu nchini Scotland imeongezeka sana katika miaka ya hivi karibuni na Waislamu wanachangia katika nyanja zote za maisha na ni muhimu kwa sehemu za Jumuiya ya Scotland.

"Tuna walimu Waislamu, madaktari, wanasheria, wamiliki wa biashara, maafisa wa polisi, wauguzi, walezi, maofisa wa baraza na katika nyanja nyingi zaidi ambazo zote zinachangia uchumi wetu kustawi.

Diwani hiyo amesema chuki dhidi ya Uislamu imekuwa ikiongezeka katika miaka ya hivi karibuni, haswa kutokana uongo unaoenezwa na mrengo wa kulia - utafiti wa hivi karibuni uligundua kuwa katika miaka mitatu iliyopita karibu nusu ya misikiti kote Uingereza ilihujumiwa na watu wenye chuki dhidi ya Uislamu.

Diwani Salamati alichukua fursa hiyo kutafakari uzoefu mbaya ambao yeye na familia yake wamekumbana nao, akisema: “Familia yangu na mimi tumepitia chuki dhidi ya Uislamu mara kadhaa.

“Mke wangu anayevaa hijabu alitemewa mate, watoto wangu wanateseka kwa ubaguzi wa rangi ndani ya shule zetu na kwenye viwanja vya soka na nimekuwa nikishambuliwa na kufukuzwa mara nyingi."

Alihitimisha: "Kwa kupitisha ufafanuzi huu tutaweza kukabiliana vilivyo na unyanyasaji wa ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya Uislamu."

3481684

captcha